The House of Favourite Newspapers

Breaking: Mbowe, Ester Matiko Wapelekwa Gereza la Segerea – Video

Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wamepandishwa kwenye gari la polisi na kupelekwa Mahabusu ya Gereza la Segerea baada ya kufutiwa dhamana katika Mahakama ya Kisutu kwa kukiuka masharti ya dhamana yao.

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa, Novemba 23, 2018 mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kutokana na maombi yaliyotolewa na upande wa mashtaka Novemba 12, uliodai washtakiwa hao wamekiuka masharti ya dhamana kwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama na kushindwa kuripoti katika kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala.

Upande wa mashtaka ulifikia hatua hiyo baada ya Mbowe kushindwa kufika mahakamani, Novemba Mosi na 8 na Matiko kushindwa kufika Novemba 8, kwa ajili ya usikilizwaji wa awali wa kesi inayowakabili.

 

Mbowe, Matiko na wenzao saba wanakabiliwa na kesi ya jinai mahakamani hapo yenye jumla ya mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi na uchochezi wa uasi ambapo watuhumiwa hao wamerudishwa rumande hadi Desemba 6, mwaka huu.

 

Hata hivyo, Wakili wa upande wa uetetezi, Peter Kibatala amesema wataukatia rufaa uamuzi huo wa mahakama.

BREAKING: MBOWE NA MATIKO Wakipelekwa Rumande

Comments are closed.