The House of Favourite Newspapers

MGOMBEA UDIWANI CHADEMA ASHAMBULIWA (Picha +Video)

Mgombea udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Kaloleni jijini Arusha, Boniface Kimaro ameshambuliwa na watu wasiojulikana huku  msaidizi wake akidaiwa kuchomwa visu usiku wa kuamkia leo katika uchaguzi wa marudio.


Kwa mujibu wa vyanzo jijini hapa, tukio hilo lilijiri kwenye kata hiyo ambapo watuhumiwa na tukio hilo hawakufahamika mara moja huku wakihusishwa na kikundi cha uhalifu.

 

Ilielezwa kuwa, mara baada ya kuvamiwa, wawili hao waliokuwa kwenye gari wakirejea majumbani, walishambuliwa ambapo hali zao zilikuwa mbaya huku mgombea udiwani akizirai.

 

Ilifahamika kuwa, polisi walifika kwenye eneo hilo la Kaloleni na kuwachukua kwenye gari kuwawahisha hospitalini.

 

RPC wa Arusha, Ramadhan Ng’anzi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema hakuna mgombea aliyechomwa kisu katika Kata ya Kaloleni.

 

“Kilichotokea ni kwamba mgombea wa kata hiyo ameshambuliwa na watu wasiojulikana na sasa hivi tumefungua kesi ili kuanza uchunguzi.

 

“Aliyechomwa kisu ni mwanachama wa CCM, ambaye alichomwa kisu eneo la Mianzini baada ya kukutana na kundi jingine ukatokea mzozo baina ya makundi hayo mawili ambapo mmoja kati ya makundi hayo akachomoa kisu akamchoma na aliyefanya hivyo tunamshiklilia hapa kituoni kwa mahojiano zaidi, lakini kwa ujumla uchaguzi katika mkoa wetu unaendelea vizuri, usalama po wa kutosha.

 

Wakati huo huo, Chadema kimetangaza kujitoa katika uchaguzi wa Kata ya Songoro, kutokana na mgombea wake na mawakala wake kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM.

Stori: Mwandishi Wetu, Arusha

Comments are closed.