The House of Favourite Newspapers

Majaliwa Azindua Uwanja wa Ruangwa

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa,  akizungumza na wananchi waliofika kushuhudia mechi ya kirafiki kati ya timu ya Simba SC na Namungo FC kwenye uzinduzi wa uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa jana (Jumamosi) Agosti 11, 2018 ambapo mchezo huo ulimalizika kwa kutofungana. 
Majaliwa (katikati) akiwa na mkewe, Mary,  akiwa na  viongozi wengine wakikata utepe kuzindua uwanja wa Ruangwa.
…Akikimbia kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa uwanja huo. 

…Akisalimiana na wachezaji wa Simba.

Wachezajiwa  Simba na Namungo FC, wakisakata kabumbu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue (kushoto) akiwa Msemaji wa Simba Haji Manara.

Mashabiki wa soka, wakiangalia mechi.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu unaojengwa na halmashauri ya wilaya ya Ruangwa na amezitaka wilaya nyingine kuiga mfano huo.

 

Uwanja huo unaoitwa Majaliwa umezinduliwa kwa mechi kati ya timu ya wilaya ya Ruangwa ya Namungo FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza na timu ya Simba SC ya Dar es Salaam, ambayo ndiyo mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara, 2018/2019.

 

Waziri Mkuu alizindua uwanja huo  Jumamosi, Agosti 11, 2018), ambapo ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Ruangwa na wananchi kwa kushiriki kikamilifu katika ujenzi huo.

 

Uwanja huo upo kitongoji cha Mtichi kata ya Nachingwea na ndiyo utakaokuwa unatumiwa na timu ya Namungo FC kuchezea mechi za nyumbani.    Amesema suala la ujenzi wa uwanja ni jambo muhimu na hata Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linahamasisha ujenzi wa viwanja katika ngazi za mikoa na wilaya ili kutoa fursa kwa wananchi hususani vijana kushiriki katika michezo, hivyo amezitaka halmashauri nyingine ziige mfano wa wilaya ya Ruangwa.

 

Akizungumzia mechi ya kirafiki kati ya timu za Simba na Namungo, Waziri Mkuu amesema “Michezo ni burudani na wananchi wanataka kuburudika, Simba chapeni kazi onesheni uwezo wenu wa mwisho ili Namungo nao waweze kupata ufundi.”

 

Pia amesema mbali na kucheza na Simba, timu hiyo ya Namungo inatarajiwa kucheza na timu ya Dodoma FC ya jijini Dodoma kesho (Jumatatu, Agosti 13, 2018) ambapo pia itacheza na timu za Yanga na Azam za jijini Dar es Salaa hivi karibuni.

 

Amesema faida ya kucheza na Namungo kucheza na  za Simba, Yanga, Azam na Dodoma FC ni kuimarishja wachezaji kwa kuwafanya wajiamini na kuondoa woga wa kupambana na timu nyingine.

 

Aidha, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuipongeza timu ya Namungo FC kwa hatua waliyofikia, kwani ilianza kwa kushiriki mashindano ya kugombea kuku, mbuzi na ng’ombe na sasa inashiriki ligi daraja la kwanza Tanzania Bara.

“Hakikisheni mnafikia lengo letu la kucheza ligi kuu,” Majaliwa alitoa wito huo kwa nguvu.

 

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi amesema kutokana na jitihada za kuboresha maendeleo zinazofanywa na Mbunge wa Ruangwa ambaye ndiye Waziri Mkuu, uongozi wa mkoa umeamua kuupa uwanja huo jina la Majaliwa ili kumuenzi.

 

Pa, Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara,  amesema timu hiyo ipo Ruangwa na benchi lake lote la ufundi wakiwemo wachezaji 27 na kwamba  ameshangazwa na wingi wa watu waliojaa uwanjani hapo.

 

“Hakuna uwanja Tanzania unaoweza kujaza watu 20,000 kwa mechi za kawaida nje ya Dar es Salaam na Mwanza. Nimeambiwa kulikuwa na tiketi 20,000 ambazo zimeisha zote,” amesema akiwa ameshangazwa na hali hiyo.

 

Comments are closed.