The House of Favourite Newspapers

Matokeo Kidato cha Sita 2020 Yapo Hapa

0

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA)  Agosti 21, 2020, limetangaza matokeo ya kidato cha sita kutokea visiwani Zanzibar ambapo kulikuwa na watahiniwa 82,440, sawa na asilimia 98.35 ya watahiniwa 84,212 waliofanya mtihani kidato cha sita Juni/Julai 2020, wamefaulu.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, amesema, watahiniwa 85,499 walisajiliwa kufanya mtihani huo, na kwamba kati yao, wasichana walikuwa 36,168 sawa na asilimia 42.30 na wavulana walikuwa 49,331, sawa na asilimia 57.70.

 

Kuangalia maokeo, fungua https://matokeo.necta.go.tz/acsee/index.htm

Amesema, kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 74,753 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 10,746.

 

Amesema, kati ya watahiniwa 85,499 waliosajiliwa kufanya mtihani huo, watahiniwa 84,212 sawa na asilimia 98.49 walifanya mtihani na 1,287 sawa na asilimia 1.51 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ugonjwa na utoro.

Amongeza kuwa watahiniwa wa shule, kati ya 74,753 waliosajiliwa, watahiniwa 74,284 sawa na asilimia 99.37 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa 32,403 sawa na asilimia 99.60 na wavulana 41,881 sawa na asilimia 99.19.

 

Kuangalia maokeo, fungua https://matokeo.necta.go.tz/acsee/index.htm

Kuhusu watahiniwa wa kujitegemea,  amesema, watahiniwa 10,746 walisajiliwa, na watahiniwa 9,928 sawa na asilimia 92.39 walifanya mtihani na 818 sawa na asilimia 7.61 hawakufanya mtihani.

 

“Jumla ya watahiniwa 82,440 sawa na asilimia 98.35 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita, wamefaulu.”

“Wasichana waliofaulu ni 35,486 sawa na asilimia 99.07 wakati wavulana waliofaulu ni 46,954 sawa na asilimia 97.81,” amesema.

 

Aliongeza kwamba mwaka 2019, watahiniwa waliofaulu walikuwa 88,069 sawa na asilimia 98.32.

 

Kuhusu ubora wa ufaulu,  amesema, madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonyesha jumla ya watahiniwa 72,230 sawa na asilimia 97.74 wamefaulu kati ya darala la kwanza hadi la tatu wakiwemo wasichana 31,786 sawa na asilimia 98.24 na wavulana 40,444 sawa na asilimia 97.35.

Kuangalia maokeo, fungua https://matokeo.necta.go.tz/acsee/index.htm

Leave A Reply