The House of Favourite Newspapers

Kocha Yanga: Kwa Bwalya, Simba Wamepata Mwamba

0

SI unakumbuka jinsi Simba walivyomnasa ‘kimafia’ kiungo matata Larry Bwalya raia wa Zambia ambaye alikuwa anaelekea kwa wapinzani wao Yanga? Sasa unaambiwa baada ya tukio hilo kuna tamko kutoka kwa kocha mwenye ‘vinasaba’ na Yanga.

 

Kocha huyo ni wa zamani wa Yanga raia wa Serbia, Milutin Sredojević ‘Micho’ ambaye amemwambia wazi Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ kuwa usajili huo wa Bwalya wamelamba dume kutokana na mchezaji huyo kuwa na uwezo mkubwa uwanjani, na matumizi makubwa ya mguu wa kushoto huku akiwa mmoja ya wachezaji wazuri nchini kwao.

 

Bwalya ni moja ya sajili walizofanya Simba kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ambapo awali Yanga walikuwa wanamuwinda staa huyo aliyekuwa akiitumikia Power Dynamos.

Mo amesema Micho amewaambia kwa kukamilisha usajili wa Bwalya wamepata mtu sahihi kutokana na kuwa na kipaji cha hali ya juu alichonacho.“Unajua Micho aliwahi kuifundisha Yanga na ni moja ya makocha wakubwa kwa Afrika kwani amewahi kuifundisha hadi Zamalek.

 

Micho ametoa tamko kuwa Bwayla ni mtu mwenye kipaji kikubwa sana.“Ana matumizi mazuri ya mguu wa kushoto na ni moja ya wachezaji wenye vipaji vikubwa kwa hiyo Simba wamepata mwamba,” alimaliza Mo.

 

Mwekezaji huyo aliongeza kuwa alizuga juu ya kauli yake kwamba timu hiyo haitasajili wachezaji wengi.“Nilikuwa nawatega tu kuhusiana na kwamba Simba haitasajili wachezaji wengi, ilikuwa ujanja tu.”

Said Ally na Wilbert Molandi,Dar es Salaam

Leave A Reply