The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Basi la Dar Express Lateketea Kwa Moto Bunju

Basi la Kampuni ya Dar Express likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam limeteketea kwa moto usiku huu wa Jumapili, Julai 8, 2018 katika eneo la Bunju Mwisho.

Aidha, chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini pia hakuna taarifa za majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa kutokana na ajali hiyo.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo amesema abiria waliwahi kushuka mara baada ya kuona dalili za moto ukiwaka kwenye taili la nyuma.

Comments are closed.