The House of Favourite Newspapers

Ghorofa Jingine la Lugumi Lanunuliwa kwa Milioni 700

0

GHOROFA  la Upanga mali ya  Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited limenunuliwa leo (Septemba 9) na kampuni ya Al- Naeen Enterprises kwa Sh700 milioni. Jengo hilo kubwa ambalo limepata mteja lipo maeneo ya Upanga.

Kampuni ya Udalali ya Yono  ndiyo inayosimamia mnada wa maghorofa hayo majengo mengine mawili yamekosa wateja kutokana na bei zake kuwa juu ukilinganisha na ukubwa wa jengo.

Akizungumza wakati wa Mnada huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Yono Scolastica Kevela amesema nyumba ambazo zimekosa wateja zinauzwa kwa  Shilingi 460 milioni ambazo zipo Mbweni JKT.

Leave A Reply