The House of Favourite Newspapers

Breaking News: JPM Ampokea Afande Sele CCM

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amempokea msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Afande Sele, ambaye amejiunga rasmi na CCM.

 

Afande Sele amejiunga na CCM leo, Alhamisi Machi 15, 2018 wakati wa hafla ya Rais Magufuli kuzindua kiwanda cha Sigara, Kingolwira, Morogoro.

Msanii huyo aliwahi kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lakini baada ya Zitto Kabwe kuhamia ACT Wazalendo, Afande naye alitimkia huko ambako alipata fursa ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro mjini mwaka 2015 lakini hakushinda.

 

Baada ya miaka kadhaa, alitangaza kujivua uanachama wa ACT Wazalendo na kusema hataki tena kufanya mambo ya siasa.

 

Na Edwin Lindege | Global Publishers

LIVE: RAIS MAGUFULI AZINDUA KIWANDA CHA SIGARA MOROGORO

Comments are closed.