The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: KAMISHNA WA TRA APATA AJALI DODOMA – PICHA

KAMISHNA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Marwa Kichere amepata ajali leo Jumanne, Septemba 11, 2018, baada ya gari lake aina ya Toyota Land Cruiser V8 kugongana na gari jingine dogo la mtu binafsi lenye namba za usajiri T 416 BTH, eneo la Nanenane, jijini Dodoma.

Inasemekana wakati gari la Kichere likipita gari jingine njiapanda ya kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), gari dogo iliyokuwa mbele ilingia ghafla kuelekea UDOM ndipo ajali ilipotokea.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza hakuna majeruhi kwa abiria wala aliyepoteza maisha kwenye ajali hiyo, lakini baada ya www.globalpublishers.co.tz kuzungumza na RPC wa Dodoma, Girres Muroto amesema hajapata taarifa za tukio hilo bado.

Endelea kufuatilia taarifa zaidi kupitia Global Habari Updates.

Comments are closed.