The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Lampard Kocha Mkuu Chelsea

FRANK LAMPARD  amesaini kandarasi ya miaka mitatu kuwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea akichukua mikoba ya Maurizio Sarri aliyejiunga na Juventus hivi karibuni.

 

Lampard mwenye umri wa miaka 41 ameondoka Derby County na kurejea ndani ya Stamford Bridge ikiwa ni miaka mitano tangu alipoondoka baada ya kuitumikia Chelsea kama mchezaji kwa miaka 13 tangu 2001 hadi 2014.

Chelsea wamemkabidhi timu Lampard ambaye aliichezea timu hiyo micheo 648, kutokana na kuaminiwa na bosi wa timu hiyo, Roman Abramovich,  ambaye alikuwa akimkubali tangu akiwa mchezaji.

 

“Nina furaha kurejea hapa kama kocha mkuu wa Chelsea, kila mmoja anafahamu mapenzi yangu na klabu hii, pamoja na historia tuliyoiweka.  Nitajikita zaidi katika kazi yangu ya kuifundisha timu, kujituma zaidi na kuiletea timu mafanikio makubwa, sina cha kusubiri,” amesema Lampard.

 

Lampard alijiunga na Chelsea mwaka 2001 akitoka timu ya vijana ya  West Ham kwa ada ya  Paundi mil. 11 mnamo 2001. Alifunga mabao 211 na kushinda mataji makubwa 11.

MATAJI

Premier League x 3

FA Cups x 4, 

League Cups x 2

Europa League x 1

Champions League x 1.

 

Comments are closed.