The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Lugola Avunja Baraza la Usalama

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelivunja Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Kamati zote za Usalama barabarani za mikoa na wilaya zote.

 

Julai 01, 2018, Rais Dkt John Magufuli alimteua Kangi Lugola Waziri wa Mambo ya Ndani akichukua nafasi ya Mwigulu Nchemba, huku akimtaka waziri huyo mpya kushughulikia sakata la Lugumi, ajali, sare za polisi, uingizwaji wa mizigo bandarini na mambo mengine ya usalama wa nchi.

Comments are closed.