The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Mama Anna Mghwira Atangaza Kujiunga CCM (Video)

Anna Mhgwira akitangaza kuhamia CCM.

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa ACT Wazalendo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Ijumaa, Desemba 8, 2017 baada ya kueleza kuwa ameridhishwa nayo.

 

Mghwira amejiunga na CCM baada kukakiribishwa na Rais Magufuli kuzungmza na kuwasalimia wananchama katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake CCM(UWT) ambapo amesema ameona si vibaya kujiunga na CCM.

 

“Kutokana na kazi niliyofanya na serikali kwa kipindi cha miezi sita, nimependa kwa utaratibu mnaofanya katika utaratibu wa vikao, ni jambo jema kwa chama na kwa jami.

 

Ninaiona CCM inayobadilika katika mkoa ninaouongoza kwa kuanza kukataa rushwa, sioni kama kuna mtu anayetaka kubaki, kwa machache hayo napenda kutamka kwamba naungana na CCM,” amesema Mghwira.

 

BREAKING NEWS: Anna Mghwira Atangaza Kujiunga CCM

Kabla ya kujiunga CCM, Mgwhira alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo ambapo aligombea Urais mwaka 2015 na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Rais Magufuli na Lowassa.

 

Mghwira, 56, ambaye anatoka mkoa wa Singida, Baba yake alikuwa diwani na kiongozi Chama cha Tanu na baadaye CCM, aliteuliwa na Rais Magufuli mnamo Jumapili June 4,2017 kuwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.

 

Mghwira anaungana na waliokuwa viongozi wenzake ndani ya ACT Wazalendo akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na Albert Msando ambao nao hivi karibuni walijiunga na CCM kwenye mkutano wa NEC huku wakiunga mkono utendaji kazi wa Rais Magufuli.

VIDEO: HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Comments are closed.