The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Mbaroni kwa Kuiba Majeneza Dar

KIJANA aliyetambulika kwa jina moja la Boniface mkazi wa Mwananyamala kwa Msisiri jijini Dar es Salaam, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa tuhuma za kuiba majeneza mawili na kuyaficha nyuma ya choo cha mkazi mwingine wa mtaa huo.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro, amesema tukio hilo limetokea kati ya ofisi mbili za kuuzia majeneza hayo ambapo ofisi moja ndiyo iliyoibiwa majeneza hayo na kuongeza kwamba jeneza moja ni la mtu mzima na moja ni la mtoto mdogo

 

“Kuna workshop mbili ambazo zinajishusisha na kutengeneza majeneza zipo sehemu moja, asubuhi mtu kaingia kwenye workshop yake akakuta majeneza mawili hayapo akaanza kufuatilia, baada ya muda akajua yapo kwenye workshop nyingine.

“Kwa hiyo kilichofanyika ni ufuatiliaji na askari wakafanikiwa kuyapata, ni suala ambalo linachunguzwa kujua kama wanadaiana au ni wizi umefanyika, ndipo sheria ifuate”, amesema Kamanda Muliro.

 

Mmiliki wa majeneza hayo Bi. Judith Carlos amesema aligundua yapo kwa jirani yake baada ya kumuahidi mtu mmoja kwamba angempa shilingi elfu 50 iwapo angemsaidia kujua nani aliyachukua, na ndipo baadaye akaambiwa mahali yalipokuwa.

“CCM Wasipoitaja CHADEMA Watamtaja Nani?”- SALUM MWALIMU

Comments are closed.