The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: MGOMBEA WA UBUNGE CHADEMA ARUDISHA FOMU (Video)

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salum Mwalimu, leo Januari 20, 2017 amerudisha fomu za kuwania kinyang’anyiro hicho katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi, Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam huku akiwataka wanachama wa chama hicho kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha muda mfupi.

Mhe. Salum ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoweza kujitokeza katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo alasiri(Jumamosi).

“Nimefarijika kwamba fomu imepokelewa na haina mapungufu yeyote yale, kwa hiyo hatuna shaka lolote katika fomu yetu kwa maana tumeikagua na kuuliza maswali katika kipengele jinsi tulivyojaza na wakatujibu tupo sahihi. Imani yangu ni kwamba hawajaona kosa ambalo wanaweza kulikalia kimya walisubiri ili lilete matatizo baadae”, alisema Mhe. Salum Mwalimu.

Katika Uchaguzi huo, Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, atachuana na aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia kabla ya kujivua uanachama na kuhamia CCM ambapo ameteuliwa tena na chama chake kupeperusha bendera.

Comments are closed.