Breaking News: Mkuu wa Mkoa Joel Bendera Afariki Dunia Muhimbili

Joel Bendera enzi za uhai wake.

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Nkaya Bendera, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiowa matibabu.

 

Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa Hospital ya Taifa ya Muhimbili, Bw. Aminiel Eligaisha amesema Bendera alipokelewa hospitalini hapo saa 6:03 mchana wa leo akitokea Bagamoyo akiwa katika hali mbaya ambapo amefariki wakati madaktari wakijitahidi kuokoa maisha yake majira ya saa 10:24 jioni hii ambapo chanzo cha ugonjwa wake hakijawekwa wazi.

 

Waziri wa Zamani wa Maliasili na Utalii, Hamis Kagasheki ameandika kwenye mtandao wake wa twitter;

“Nimepokea kwa mstuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Ndg Joel Bendera. Alilitumikia Taifa letu kwa jitihada kubwa. Kwa kutaja machache, aliwahi kuwa Mbunge, Naibu Waziri, Mkuu wa Mikoa kadha nk. Pole zangu kwa family, ndugu, rafiki,wa marehemu. Rest in peace Joel,” ameandika Kagasheki. 

Katika uhai wake, Bendera amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo.

Fuatilia Taarifa ya Habari ya Global TV Online saa 2:00 usiku huu kwa taarifa zaidi.


VIDEO: MSIKIE OFISA WA MUHIMBILI AKIZUNGUMZAIA MSIBA HUO

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment