The House of Favourite Newspapers

Polepole Afafanua CCM Kufuta Uchaguzi Baadhi ya Maeneo (Video)

0

KATIBU wa Itikadi na  Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amefafanua kuhusu kufutwa na kurudiwa upya katika baadhi ya maeneo yaliyovunja utaratibu wa uchaguzi unaoendelea katika chama hicho.

 

Alifafanua kwamba uchaguzi huo umefutwa kwa vile wagombea hawakao maeneo husika na walichaguliwa kwa kutofuata misingi ya CCM.

 

“Kuna wanachama wachache ndani ya chama chetu wanaofuata utaratibu wa zamani, CCM hii ni mpya na inayofuata misingi ya chama na hakuna makundi ya sasa ndani ya chama na jukumu letu ni moja ni kujenga chama,” alisem, Polepole.

 

Polepole amesema hayo leo alipokutana na waandishia wa habari ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. Aliongeza kuwa kuwa viongozi waliosimamia uchaguzi huo uliopita watasimamiwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

 

Kada huyo wa CCM alisema chama chake kimejipanga kuhakikisha kuwa wanafanya uchaguzi ambao utazingatia na kuendana na matakwa ya CCM mpya kwa kusimamia misingi ya mageuzi ya chama hicho.

 

Leave A Reply