The House of Favourite Newspapers

Mkurugenzi Global Ahudhuria Mahafali ya Mwanaye Elite Sprints

0
Mtoto Emmanuel Samson akiwa katika pozi na zawadi zake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers ambaye ni mama mzazi wa Emmanuel, Lydia James, akiwa na mwanaye.
Mtoto Emmanuel akiwa na keki yake maalum iliyokuwa imeandaliwa.
Wanafamilia ya Emmanuel wakiwa katika picha ya pamoja.
Dada wa Emmanueli aitwaye Iman Aaron akimlisha keki.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, James Kiambati, akiwa katika picha ya pamoja na mama yake Emmanuel.
Ofisa Elimu Kata ya Goba, Jacob Gulied, akimkabidhi cheti mtoto Emmanuel.
Watoto waliohitimu masomo ya awali wakiwa pamoja.

MKURUGENZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd inayochapisha magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa na Championi, Lydia James Bukumbi, jana alihudhuria mahafali ya mwanaye, Emmanuel Samson, aliyehitimu masomo ya elimu ya awali (chekechea) katika shule ya Elite Sprints, iliyoko Goba jijini Dar.

Katika hafla hiyo, mkurugenzi huyo alimwandalia keki maalum mwanaye yenye ujumbe wa kumpongeza na kumtia moyo ikiwa ni njia ya kushiriki naye furaha hiyo.

“Kupiga hatua moja kwenda nyingine ni jambo la heri na la kumshukuru Mungu, nimefurahi kuona mwanangu anahitimu masomo ya elimu ya awali, namuomba Mungu amjalie afya njema, hekima na busara katika kukua kwake ili mwakani aweze kujiunga na masomo ya elimu ya msingi. Pia ninayo heshima na shukurani za dhati kabisa kwa walimu wa shule hii kwani mafundisho yao yanawalea watoto kielimu na nidhamu bora. Mungu awabariki,” alisema Lydia.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply