The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Rais Magufuli Afiwa na Dada Yake

Marehemu Monica Joseph Magufuli enzi za uhai wake.

Dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Monica Joseph Magufuli amefariki dunia asubuhi leo Agosti 19, 2018 katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu.

Rais Magufuli jana alifika katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza kumjulia hali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipomtembelea kumjulia hali dada yake, Monica Joseph Magufuli jana ambapo alikuwa amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Bugando mkoani Mwanza.

 

 

Comments are closed.