Breaking News: Spika Ndugai Kusimamishia Mshahara wa Tundu Lissu – Video

SPIKA wa Bunge Job Ndugai amesema ipo haja ya kusimamisha Mshahara na Malipo yote ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kutokana ana Ofisi yake kutokuwa na Taarifa sahihi ya mahali alipo kwasasa na anachokifanya huko.

 

Spika Ndugai ametoa taarifa hiyo leo Alhamisi, Februari 7, 2019 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu Muongozo wa Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ ambapo amesema Mbunge huyo hayupo Hosipitali,Hayupo Bungeni na hayupo Tanzania wala hajulikani anafanya kitu gani huko aliko hivyo hana sababu ya kuendelea kulipwa.

 

“Tundu Lissu anazunguka huku anasemekana anaumwa, ni lini Bunge litasitisha mshahara wake kwa sababu ameshapona na ameendelea kuzunguka huko na huko akitukana Bunge na Serikali,” amesema Msukuma.
Akijibu mwongozo huo, Nduhai amesema, “Hili la ndugu yetu Lissu linatakiwa kuliangalia kipekee, Mbunge hayupo jimboni kwake, hayupo hapa Bungeni tunapofanya kazi, hayupo Hospitalini, hayupo Tanzania, na taarifa zake Spika hana kabisa, wala hajishughulishi kumwandikia spika kwamba yupo mahala flani, au nafanya hivi.
“Kama ni mgonjwa hakuna hata taarifa zozote kutoka kwa daktari, halafu unaendelea kumlipa malipo mbalimbali, nadhani ipo haja ya kusimamamisha malipo ya aanina yoyote ile, mpaka ambapo tutapata taarifa za yuko wapi na anafanya nini,” alisema Ndugai.

VIDEO: NDUHAI AKIZUNGUMZA

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment