The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: TRUMP ATEMBELEA KOREA KASKAZINI LEO – VIDEO

Rais wa Marekani, Donald Trump leo Juni 30, 2019 amekuwa Rais wa kwanza wa Marekani kukanyaga ardhi ya Korea Kaskazini akiwa madarakani na kukutana na Rais wa nchi hiyo, Kim Jong-un na  kufanya tukio la kihistoria baada ya kukutana, kupeana mikono.

Wawili hao walikutana mpakani mwa Korea Kaskazini na Kusini kabla ya mkutano na waandishi wa habari wakiwa na kiongozi wa Korea Kusini Moon Jae-in

Akizungumza na waandishi, Trump ameeleza kuwa amefurahi sana kuruhusiwa kuvuka mstari wa mpaka kati ya Korea Kaskazini na Kusini na hiyo inaonesha kuwa uhusiano kati yao na mataifa yao umekuwa mzuri sana

Kim pia ameonesha kufurahishwa na mkutano huo ambao amesema anaamini unaenda kufuta uhasama wa nyuma na kuleta wakati ujao wenye mafanikio

Hata hivyo, Rais Trump amesema vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini viko pale pale licha ya ziara hiyo ya kihistoria na mazungumzo yaliyofanyika.

Katika mkutano huo Rais Trump amepongeza Korea Kaskazini kwa kutofanya majaribio ya makombora ya umbali mrefu katika kipindi cha karibuni. Amesema majaribio yanayofanyika hivi sasa ni ya kawaida ambayo kila nchi inafanya.

Trump amesema anaweza kumkaribisha Kim Marekani hata hivi sasa na kumtaka aende wakati ukiwa sahihi. Na inaaminika pia kuwa Kim amemkaribisha Trump Pongyang katika clip moja kutoka kwenye mkutano huo uliodumu kwa takribani saa 1.

Comments are closed.