The House of Favourite Newspapers

Breaking: Teddy Mapunda Afariki Dunia

0

HABARI zilizotufikia hivi punde, Mkurugenzi wa Service and Montage Limited, Teddy Hollo Mapunda, maarufu ‘Dada Teddy’ amefariki usiku huu katika hospital ya Agakhan alikokimbizwa kwa matibabu kutokana na mshtuko wa moyo.

 

Mmoja wa watu wa karibu ambae alikua na marehemu Teddy wakipata futari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam amesema;

 

“Teddy tulikua nae tunafuturu, lakini alinyanyuka akaenda chooni alipotoka akasema anasikia kizunguzungu huku ameshika kichwa, gafla akaanguka, tumemkimbiza Agakhan, madaktari wamejitaidi sema ndio hivyo,” amesema.

 

Teddy amejipatia umaharufu mkubwa kutokana na kupamba kwenye Dhifa mbali mbali za Kitaifa, ndiye aliyepamba Uwanja wa Uhuru na Chato siku ya msiba wa aliyekua Rais wa Awamu ya Tano John Magufuli.

 

Teddy pia amekua mstari wa mbele kuhamasisha wadau wa Michezo kuichangia na kufanikisha ushindi wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ katika michuano mbali mbali ya kimataifa.

Leave A Reply