The House of Favourite Newspapers

Breaking: Waziri Wa Kazi Auawa Kwa Kupigwa Risasi Na Mlinzi Wake Nyumbani Kwake

0
Charles Okello Engola ni Waziri wa Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda wa Nchini Uganda.

Charles Okello Engola ni Waziri wa Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda wa Nchini Uganda ambaye anadaiwa kuuawa asubuhi ya hii leo Mei 02, 2023 kwa kupigwa risasi na mlinzi wake.

Kwa mujibu wa Naibu Msemaji wa Polisi, Luke Owoyesigire, tukio hilo limetokea asubuhi ya leo.
Imeelezwa kuwa Waziri Okello alikuwa anatoka nyumbani kwenda kazini na ndipo ghafla mlinzi wake binafsi akampiga risasi kisha akaanza kupiga risasi juu huku akikimbiakimbia mitaani.

Msemaji huyo ameeleza kuwa mlinzi huyo amesikika akisema hajalipwa mshahara kwa muda mrefu.
“Ni kweli. Nendeni Kyanja. Mlinzi amemuua bosi wake,” Luke Owoyesigire.

Leave A Reply