The House of Favourite Newspapers

Maandamano Mapya Yaanza Kenya: Polisi Wamwagwa Kila Kona, Waandamanaji Wafunga Barabara Kwa Mawe

0

Baada ya upinzani kutangaza maandamano mapya nchini Kenya, idadi kubwa ya Polisi imemwagwa katika maeneo mbalimbali jijini Nairobi.
Polisi wamewekwa kwenye maeneo makuu ya kuingia katika Jiji la Nairobi na kutoka ikiwa ni pamoja na Barabara za Uhuru Highway – Haile Mtaa wa Selassie na baadhi ya maeneoya Ngara.
Hali hiyo pia imeshuhudiwa katika barabara ya Ngong.
Vizuizi pia vimewekwa katika barabara inayoelekea katika Ofisi za Ikulu huku maafisa wa Polisi wakionekana katika barabara zinazoelekea kwenye Ikulu hiyo.
Katika baadhi ya meneo ya mji wa Kisumu ambao ni ngome ya kiongozi wa upinzani, Raila Odinga tayari maandamano yamekwishaanza huku waandamanaji wakiripotiwa kufunga barabara kwa mawe na kuwasha moto barabarani.


Katika taarifa aliyoitoa kuhusu maandamano ya Muungano wa Azimio la Umoja, Kamanda Mkuu wa Polisi Kanda ya Nairobi, Adamson Bungei alidai kuwa Azimio hawakuonesha kuwa na malengo mazuri katika maandamano yao yaliyopita akasema hawafai kuongoza maandamano.
Kwa upande wake, Rais William Ruto ameapa kutumia mamlaka yote aliyonayo kuhakikisha kuwa maandamano yaliyopangwa hayageuki kuwa vurugu na ghasia.
Hata hivyo, Raila Odinga ameapa kuwa maandamano lazima yaendelee kwani anasema Serikali ya Rais Ruto haiku tayari kushughulikia masuala, mkiwemo kushugulikia gharama za maisha, kufunga seva za matokeo ya uchaguzi, kufanyika kwa mageuzi katika utendaji wa Tume ya Uchaguzi.

ITAKULIZA! BICHUKA HOI, MACHO HAYAONI, MAISHA MAGUMU, MKE AFUNGUKA SHIDA WANAZOPITIA | KATA

Leave A Reply