British Council yakabidhi mpango wa kufundisha Kiingereza
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk. Leonard Akwilapo, akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Shughuli zikiendelea.
Kutoka kushoto ni mdau wa elimu kutoka British Council, Richard Sunderland, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo na Kamishna wa Elimu, Dk. Edicorp Shirima.
Baadhi ya walimu wa shule za sekondari hapa nchini waliohudhuria hafla hiyo.
Wadau wa elimu wakifuatilia hafla hiyo.
Kitengo cha Tehama kikiwa kazini.
Waratibu wa mpango huo wakizungumza jambo.
Wadau wa elimu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika hafla hiyo.
Wadau wakiendelea na shughuli mbalimbali.
SHIRIKA la Misaada la Uingereza lijulikanalo kama British Council jana limekabidhi mpango wa kuimarisha ufundishaji wa lugha ya Kiingereza katika shule za sekondari hapa nchini.
Mpango huo umekamilika na kukabidhiwa kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Naibu Katibu Mkuu Dk. Leonard Akwilapo jana katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Akwilapo alisema kuwa mpango huo ulifanyika kwa majaribio ambapo mikoa mitano ya Tanzania Bara ilihusishwa, ambayo ni, Dar es Salaam, Mbeya, Pwani, Kagera na Arusha.
Alifafanua kuwa mpango huo umewawezesha wanafunzi wa kidato cha kwanza kila wanapotoka shule za msingi kupata masomo ya awali ya lugha ya Kiingereza kwa muda wa miezi sita.
Aliongeza kuwa lugha ya Kiingereza ni daraja linalounganisha ulimwengu japokuwa sera ya elimu ya mwaka 2014 inatambua lugha ya Kiswahili na Kiingereza kuwa ni lugha za kufundishia kwa ngazi zote kuanzia chini hadi chuo kikuu huku lugha ya Kiswahili ikiendelea kuwa lugha ya kufundishia shule za msingi kama sera inavyoeleza.
Aidha mratibu wa mradi huo, Naomi Swai, amesema kuwa mpango huo umeleta mafanikio makubwa kwa kuwapatia waalimu mafunzo ya kufundisha lugha hiyo na kupata vitabu vitakavyosaidia njia za kufundishia Kiingereza ambapo zaidi ya walimu 2,485 na wanafunzi 65,000 wamefanikiwa katika mpango huo kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013.
Na Denis Mtima/Gpl.