The House of Favourite Newspapers

Buchosa Mpya Sasa Kuwagusa la Pili Hadi la Saba Mpaka Sekondari

0

Kampeni ya Buchosa Mpya, Peleka Mtoto Shule imeendelea jana katika Kata ya Kasisa, Nyakasungwa na Bukokwa ikiwa ni mwendelezo wa kugawa sare za shule kwa wanafunzi wanaotoka familia zisizojiweza pamoja na kuwapa madaftari wanafunzi wote wa darasa la kwanza katika jimbo zima la Buchosa.

Mratibu wa Kampeni hiyo, kutoka ofisi ya mbunge wa Buchosa, Charles Matiku amesema ugawaji wa sare na madaftari ni utekulezaji wa ahadi ya Mbunge Eric Shigongo ambayo aliiahidi wakati wa kampenizake kusaidia elimu.

Matiku amesema katika kipindi kifupi cha uongozi wake Shigongo amefanya mambo mengi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa mabati, saruji za ujenzi wa shule na zahanati katika kata mbalimbali na utengenezaji wa barabara katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

Matiku ameongeza kuwa zoezi la ugawaji wa sare na madaftari ni zoezi endelevu kwani awamu inayofuata itakuwa kwa wanafunzi wa darasa la pili hadi darasa la saba pamoja na shule za sekondari katika jimbo zima la Buchosa.

 

 

 

 

 

 

 

 

MBUNGE SHIGONGO Awapa SOMO WAZAZI – “USIMPE Simu MTOTO, Usimruhusu AANGALIE TV Muda WOTE”

Leave A Reply