The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Apewa Saa 24 Kujiuzulu

0

Wabunge wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepiga kura kumuondoa madarakani Waziri Mkuu, Sylvestre Ilunga Ilukamba na wamempa saa 24 ajiuzulu.

 

Waziri Ilukamba ambaye anatuhumiwa kuwa mshirika wa Rais wa zamani Joseph Kabila pia, anatuhumiwa kwa utendaji kazi mbovu.

 

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Congo Waziri kulazimishwa kujiuzulu. Inaelezwa, Rais FĂ©lix Tshisekedi atateua Baraza jipya la Mawaziri ambao ni watiifu kwake.

 

Serikali ya DRC, ina Mawaziri 60 ambapo wengi wanatoka katika Chama cha Joseph Kabila huku 23 wakitoka katika Muungano wa Rais Felix Tshisekedi.

Leave A Reply