The House of Favourite Newspapers

Bunge Lamchagua Cyril Ramaphosa Kuwa Rais wa Afrika Kusini

BUNGE la Afrika Kusini limemchagua Mwenyekiti wa chama tawala cha ANC Cyril, kuwa Rais wa mpito wa nchi hiyo, mpaka pale uchaguzi utakapofanyika baada ya rais wa taifa hilo Jacob Zuma kujiuzulu.

 

Zuma alikuwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa chama chake cha ANC kilichomtaka ajiuzulu kutokana na madai kadhaa ya ufisadi, lakini alikana kufanya makosa yoyote. Alijiuzulu mara moja jana jioni licha ya kusema hakubaliani na uamuzi wa chama.

Comments are closed.