The House of Favourite Newspapers

Burna Boy Atajwa Orodha ya Watakaotumbuiza Kwenye Tuzo za Grammy

0

Siku chache tangu waandaaji wa Tuzo za Grammy wawatangaze wasanii watakao-perform kwenye tuzo hizo mwaka huu na kuwataja Billie Eilish, Olivia Rodrigo na Dua Lipa, orodha ya pili ya wasanii watakao-perfom imetoka huku staa wa Nigeria, Burna Boy naye akilamba shavu.

Katika taarifa mpya iliyotolewa na waandaaji wa tuzo hizo, jana Jumapili, Januari 21, 2024, wasanii wengine waliotajwa mbali na Burna Boy ni Travis Scott na Luke Combs ambapo event ya utoaji wa tuzo hizo inatarajiwa kufanyika Jumapili ya Februari 4, 2024 huku wasanii wengine wakitarajiwa kutangazwa siku chache zijazo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Trevor Noah ndiye atakayekuwa host wa event ya utoaji wa tuzo hizo kwa mwaka huu.

Mbali na kuwa mtumbuizaji, Burna Boy pia amekuwa nominated kuwania tuzo 4 mwaka huu, Best Global Music Album (I Told Them…), Best African Music Performance (City Boys), Best Global Music Performance (Alone) na Best Melodic Rap Performance (Sittin’ On Top of the World).

Burna Boy amewahi kushinda tuzo moja ya Grammy mwaka 2021 kupitia kipengele cha Best Global Music Album (Twice As Tall).

Leave A Reply