The House of Favourite Newspapers

Burundi Yiishutumu Rwanda kwa Jaribio la Kumuua Mshauri Mkuu wa Rais Nkurunzinza

cyb9emgxuaakch0

Burundi imemlaumu jirani wake Rwanda kwa kupanga jaribio lililofeli la kutaka kumuua mshauri mkuu wa rais Pierre Nkurunziza.

Msemaji wa polisi Pierre Nkurukiye, alisema kuwa maagizo yalitumwa kutoka nchini Rwanda kwa wapanganji walio katika jeshi la Burundi ya kumuua Willy Nyamitwe.

Bwana Nyamitwe, alipata majeraha madogo kwenye mkono wake huku mlinzi wake mwengine akijeruhiwa kwenye shambulio hilo siku ya Jumatatu usiku, kwa mujibu wa maafisa. Rwanda haijajibu madai hayo. Awalia ilikana madai kama hayo.

_92710066_e3656687-055d-4d9f-8f8b-d213e1835cc5 Nyamitwe (kulia) akiwa na rais Nkurunzinza.

Bwana Nyamitwe alivamiwa alipokuwa akirudi nyumbani mwake Magharibi mwa Kajaga huko Burundi. Hii si mara ya kwanza Nyamitwe kuvamiwa, tovuti ya habari inayounga mkono serikali imesema.

Mwezi Julai mbunge katika bunge la Afrika ya Mashariki rais wa Burundi Hafsa Mossi, aliuawa kwa kupigwa risasi mjini Bujumbura kwenye shambulizi ambalo serikali ilisema liliagizwa na Rwanda.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedorora tangu mwaka uliopita. Burundi inamlaumu Rwanda kwa kuwapa makao maafisa wa kijeshi waliopanga mapinduzi ya kijeshi dhidi ya bwana Nkurunziza mwezi Mei mwaka 2015 baada ya kutangaza kuwa alikuwa akiwania muhula wa tatu. Zaidi ya watu 500 wauwawa na wengine takriban 270 kuukimmia mzozo uliopo nchini Burundi.

Comments are closed.