The House of Favourite Newspapers

Bwire: Tunawaondoa Simba FA

0

RUVU Shooting kuelekea mchezo wao wa leo Jumatano wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (FA) utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar dhidi ya Simba SC, wamesema kuwa wapo tayari kulishangaza taifa.


Akizungumza na Champion
Jumatano, Mkuu wa Idara ya Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema kuwa, wamefanya maandalizi makubwa kuelekea mchezo huo ili kuhakikisha wanamuondoa bingwa mtetezi wa kombe
hilo, Simba.


“Tumejipanga kuhakikisha tunabadili
fikra za watu wengi kwamba timu yoyote itakayo kutana na Simba au Yanga basi haitoweza kupata matokeo, Ruvu ni timu kubwa yenye wachezaji wenye ubora wa hali ya juu hivyo wajiandae kula kipigo kizuri kutoka kwetu.

 


“Nawaambia Simba waje kucheza
mpira, wasithubutu kuja na matokeo yao mfukoni kwa sababu ni kitu ambacho kitakuja kuwaletea madhara makubwa sana baada ya dakika 90 za mchezo.”

STORI: NAILA SHOMARI | CHAMPIONI JUMATANO


Leave A Reply