The House of Favourite Newspapers

Mwandishi Imelda Mtema Apongezwa Kunyakua Tuzo – Video

0


Mwandishi mkongwe na mahiri wa Global Group anayeripotia magazeti ya Global Publishers na Kituo cha Runinga ya Mtandaoni cha Global TV Online, amefanyiwa hafla fupi ya kumpongeza kufuatia kung’ara katika tuzo maalum zilizotolewa na mtangazaji Dina Marious.

Hafla hiyo ndogo imefanyika katika ofisi za Global Group, Sinza Mori ambapo mwanahabari huyo alifanyiwa mahojiano maalum na Global TV pamoja na +255 Global Radio na kueleza furaha aliyokuwa nayo kutokana na kunyakua tuzo hiyo.

 

Mbali na kuelezea furaha yake, pia Imelda amefunguka mambo mbalimbali kuhusu changamoto alizowahi kukutana nazo wakati akitekeleza majukumu yake ya kiuandishi wa habari, likiwemo tukio la supastaa Wema Sepetu kumfanyia timbwili ofisini baada ya kuandika habari ambayo haikumpendeza!
Pia amesimulia jinsi alivyowahi kukimbizwa na kisu umbali mrefu, baada ya kwenda ku-balance stori iliyokuwa inamhusu staa wa zamani, Aisha Bui miaka kadhaa iliyopita.
Mahojiano kamili tazama Global TV Online!

Leave A Reply