The House of Favourite Newspapers

CAG: Deni la Serikali Lafikia Shilingi Trilioni 82.25 sawa na ongezeko la 15%

0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere leo Machi 28, 2029 akibidhi ripoti ya utendaji kazi wa serikali na mashrika mbalimbali ya umma na binafsimwaka 2022/2023 IKulu ya Chamwino, Dodoma amesema kufikia Juni 30, 2023 deni la serikali lilikuwa shilingi trilioni 82.25, sawa na ongezeko la asilimia 15 kutoka shilingi trilioni 71.31 kwa mwaka 2021/2022. Deni hilo linajumuisha deni la ndani la shilingi trilioni 28.92 na deni la nje la shilingi trilioni 53.32.”

Kipimo cha deni la serikali kinachotumia pato la Taifa kinaonesha kuwa deni hili ni himilivu. Halikadhalika uwiano wa kulipa madeni na mauzo ya nje ni asilimia 12.7 chini kidogo ya kiwango cha ukomo cha asilimia 15 na uwiano wa malipo ya madeni na mapato ni aslimia 14.3, chini kidogo ya kiwango cha ukomo elekezi cha asilimia 18”

Leave A Reply