The House of Favourite Newspapers

Hasara ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Yapungua kwa Asilimia 94

0

“Kwa mwaka wa fedha 2022/23 Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limepata hasara ya shilingi Milioni 894. Hasara hii imepungua kwa asilimia 94 ukilinganisha na hasara ya shilingi Bilioni 19.2 katika mwaka uliopita.”

“Shirika limetengeneza hasara hii licha ya kupokea ruzuku ya shilingi Bilioni 4.55 na kuonesha shilingi Bilioni 4.4 ikiwa ni sehemu ya ruzuku kama mapato yake kwa mwaka 2022/23”

Hayo yamezungumzwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere wakati akikabidhi ripoti ya utendaji kazi wa serikali na mashrika mbalimbali ya umma na binafsi

Leave A Reply