The House of Favourite Newspapers

Cannavaro Meneja Mpya Yanga

YANGA wamemwambia Nadir Haroub ‘Cannavaro’ mziki wa Emmanuel Okwi na Meddie Kagere wa Simba hatauweza msimu huu badala yake ajiandae kisaikolojia kuwa meneja tu.

 

Hiyo inamaanishwa kwamba Hafidh Saleh ambaye ameshikilia nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka 10 atapangiwa majukumu mengine kwenye benchi la ufundi.

 

Cannavaro akiwa nahodha wa timu hiyo amenyanyua makombe matano kati ya hayo matatu ya Ligi Kuu Bara, moja la Kagame na Ngao ya Jamii moja.

 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema wameamua kubadilisha benchi la ufundi kwa kumpa Cannavaro nafasi ya umeneja na Hafidhi atakuwa mratibu lengo ni kuboresha benchi la ufundi kwani awali kwenye michuano ya kimataifa walikuwa hawana mtu sahihi wa kufuatili vitu mbalimbali vya michuano ya kimataifa pindi walipokuwa wakishiriki.

 

Alisema baada ya kuona hivyp wakafikia muafaka kwamba Hafidhi apewe nafasi ya uratibu kwani anamudu kushughulikia ishu hizo ili kuepukana na adhabu ambazo zinaweza kutolewa na Shirikisho la Soka Afrika’Caf’.

 

Pia kocha wa makipa Juma Pondamali hatokuwa sehemu ya kikosi hicho kuanzia sasa na sasa wanatafuta mbadala wake mwenye uwezo zaidi.

“Tumeamua kuimarisha benchi la ufundi kwa kumpa umeneja Cannavaro na Hafidhi atakuwa mratibu wa timu, pia tumeachana na Pondamali ambapo sasa tunatafuta mbadala wake,” alisema Nyika.

 

Alipotafutwa Cannavaro kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Sipo Dar, hapa ninapoongea na wewe nipo Hospitali ya Mnazi Mmoja huku Unguja, Zanzibar nilipokuja leo (jana) kwa ajili ya kumuuguza mama yangu.

 

“Hivyo sitaweza kuzungumzia hilo kwa hivi sasa nivumilie nitakupigia tutaongea vizuri, mama yangu amepata ‘stroku’ mguuni na mkononi,” alisema Cannavaro.

Comments are closed.