The House of Favourite Newspapers

Cannavaro: Nini Kiongera, mleteni hata Sserunkuma

0

WAKATI Simba ikipanga kumrejesha kiungo mshambuliaji Paul Kiongera, beki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema hata klabu hiyo ikimrudisha straika Danny Sserunkuma wataifunga tu.

Simba inataka kumrejesha Kiongera katika kikosi chake akitokea KCB ya Kenya anakocheza kwa mkopo ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake. Kiongera raia wa Kenya alipelekwa KCB mwaka jana, pia Simba iliachana na Sserunkuma raia wa Uganda msimu uliopita baada ya kushindwa kung’ara.

Baada ya kupenyezewa data hizo, Cannavaro aliliambia Championi Jumamosi kuwa: “Nasikia Simba wanataka kumrudisha Kiongera, jambo zuri lakini wajue hatofanya lolote na hata wangemrudisha Sserunkuma ni sawa na bure tu.

“Tutaendelea kuifunga Simba kwani hawana kikosi imara kulinganisha na sisi, kama unavyoona tunaendeleza ushindi tu katika mechi zetu kutokana na usajili imara uliofanywa na viongozi.”

Jumamosi iliyopita Yanga iliifunga Simba mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabao yaliyofungwa na Amissi Tambwe na Malimi Busungu.

Leave A Reply