CASTO: SIONI SABABU YA KUBAKI NA TATTOO YA TUNDA

Casto Dickson

BAADA ya kumwagana na mpenzi wake wa zamani Anastazia Kimaro ‘Tunda’ mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson amesema kwamba haoni sababu ya kuendelea kuitunza tattoo yenye jina la mrembo huyo kwenye mwili wake.  Akizungumza na Showbiz Xtra, Casto ambaye awali alikufa na kuoza kwenye penzi la Tunda hadi kujichora Tattoo yenye jina la mrembo huyo na kudai kuwa hata itokee nini hataifuta kwenye mwili wake lakini sasa anaonekana kubadili ‘gia angani’.

“Mimi siyo mtu wa kuongelea haya mambo na sikupanga kabisa kuongelea hili suala, lakini kwa kuwa umeniuliza acha nikujibu, iko hivi mimi na yule msichana tulishaachana na kila mtu anafanya yake sasa hivi, sasa sioni sababu ya kuendelea kukaa na Tattoo ya mtu ambaye sipo kwenye uhusiano naye,’’ alisema Casto.

Penzi la wawili hao lilianza kuvuma ghafla baada ya picha na video zao za kimahaba kusambaa mitandaoni, ambapo mara kadhaa Casto alionekana kumposti Tunda kwenye akaunti yake ya Instagram na kusisitiza kuwa atamuoa.

MEMORISE RICHARD

Loading...

Toa comment