The House of Favourite Newspapers

CAVS YAICHAPA BULLS KWA POINTI 104-101

JORDAN Clarkson na Alec Burks kila mmoja alifunga pointi 18, Cedi Osman akaongeza 17 na Cleveland Cavaliers ikamaliza mwendo wa kupoteza michezo sita mfululizo kwa kuichapa Chicago Bulls 104-101, katika Ligi ya NBA.

Matthew Dellave dova yeye alikuwa na pointi 16 na Rodney Hood aliongeza 14. Lauri Markkanen aliiongoza Chicago kwa kufunga pointi 21 na ribaundi 12, wakati Zach LaVine alikuwa na pointi 17 na ribaundi 12. Sasa Bulls imepoteza mechi tatu mfululizo, na 13 kati ya 14.

 

Larry Nance Jr. wa Cavs hakufunga pointi yoyote kwa dakika 17 akitokea benchi katika mchezo wake huo wa pili baada ya kupona majeraha yake ya goti la kulia.

 

Lakini kwa upande wa Bulls, imefahamika kuwa Rookie F Chandler Hutchinson, aliyeumia mfupa wa mguu wake wa kulia katika mchezo wa Alhamisi iliyopita dhidi ya Atlanta Hawks, atakuwa nje ya dimba kwa angalau mwezi mmoja. Awali ilionekana kama tatizo ni dogo lakini sasa litamweka nje kwa wiki nne

Comments are closed.