The House of Favourite Newspapers

CCM Walivyotesti Mitambo Mitaa ya Dodoma Leo

0

Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo walionesha jeuri ya chama chao wakati wakifanya maandalizi ya kumpokea Mwenyekiti wa Chama hicho na Mgombea Uraisi, Dkt John Pombe Magufuli anayetarajiwa kuzindua kampeni za chama hicho hapo kesho.

Kampenzi hizo zinatarajiwa kuzinduliwa kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini hapa ambapo pamoja na viongozi wa chama hicho wasanii mbalimbali wanatarajiwa kufanya yao.

Katika maandalizi hayo ya kumpokea Dkt. Magufuli wafuasi hao na wasanii walizunguuka mitaa mbalimbali ya jiji la Dodoma wakiongozwa na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.

 

Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akiwaongoza wafuasi wa CCM katika maandalizi ya kumpokea mgombea Uraisi kupitia chama hicho, Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Msafara wa wafuasi wenye bodaboda ulivyonogesha mambo.

 

Petit Man na Dyna Nyange nao walikuwepo kwenye msafara wa kuzunguuka viunga vya Jiji la DOM.
Muigizaji wa vichekesho, Fatuma Mzuzuri a.k.a Asha Boko baada ya kuchoka kupiga jalamba alijisalimisha kwa kudandia kirikuu iliyokuwa kwenye msafara huo.
Rachel Kizunguzungu (kulia) na Linnah Sanga nao walipiga jalamba mtaani.                                                             
Msanii wa Bongo Muvi Blandina Chagula a.k.a Johari naye kama kawa.
Wasanii wa Bongo muvi kutoka kushoto, Petit Man, Aunty Ezekiel na Kajala Masanja nao wakiwa kwenye msafara.                                                                                                                                                                            HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL        
Leave A Reply