The House of Favourite Newspapers

Cedric Kaze Azua Utata Yanga SC

0

KOCHA mkuu mpya wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze ambaye alitarajiwa kutua usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, sasa atatua Jangwani Jumatano ijayo akitokea Canada kwa ajili ya kuanza kazi.

 

Awali iliripotiwa kuwa, Kaze angetua nchini juzi Jumamosi, Alfajiri kwa ajili ya kuanza kazi Yanga lakini Ijumaa mchana habari kutoka ndani ya Yanga zilisema kocha huyo atatua Jumatano na kuanza kazi katika kikosi hicho ambacho kipo kambini huko Avic Town, Kigamboni jijini Dar.

 

Kikizungumza na Championi Jumamosi, chanzo kilisema kuwa, kimefanya mawasiliano na kocha na kumwambia kuwa atatua nchini Jumatano ijayo tayari kwa kuanza kazi.

 

“Kocha atakuja Jumatano ijayo akitokea Canada, akifika tu atamaliza masuala yake binafsi na uongozi, baada ya hapo ataanza kazi,” kilisema chanzo hicho.Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema:

 

“Siwezi kukueleza kwamba atakuja muda gani lakini matarajio yetu ni kuweza kumpokea siku ya kesho ‘leo’ kwa ajili kuanza majukumu yake.

 

“Sitaki ni kuhakikishie lakini hayo ndiyo matarajio yetu makubwa juu yake na atakuja akitokea Canada lakini kwa jambo lolote juu yake likitokea basi uongozi utaweka wazi.”

 

WILBERT MOLANDI NA IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Leave A Reply