The House of Favourite Newspapers

CEED TANZANIA YATOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI

Mfanyabiashara wa kuku hapa nchini, Elizabeth Swai akileza jambo.
Mwakilishi kutoka CEED Tanzania, Fred Laiser akizungumza na wanahabari.
Baadhi ya wajasiriamali waliohudhuria wakifuatilia kwa makini somo la usimamizi wa wa biashara zao.

 

 

Kituo cha Ujasiriamali na Maendeleo ya Utendaji (CEED), ya wakutanisha wafanyabiashara mbalimbali wa mazao ya kilimo na usindikizaji vyakula katika hafla iliyolenga kutoa mafunzo ya usimamizi, maarifa ya biashara, utayari wa uwekezaji na fursa za mtandao.

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari, mwakilishi kutoka CEED , Fred Laiser amesema lengo la hafla hiyo ni kutoa elimu kuhusu usimamizi wa biashara zao na kuwakutanisha wajasirimali kutoka ndani na nje ya nchi ili kujifunza mengi zaidi.

 

 

“Sisi CEED kazi yetu ni kuwainua wajasiriamali mbalimbali nchini hasa wa mazao ya kilimo pamoja na mifugo.Leo tupo hapa kwa ajili ya kuwapa elimu ya usimamizi wa biashara zao hasa zinapokuwa kubwa kwasababu biashara inapokuwa kubwa changamoto nazo zinaongezeka”,alisema Fred.

 

 

Kwa upande wake mmoja wa  washiriki kutoka Tanzania, Bi Elizabeth Swai mjasiliamali wa biashara ya kuku alisema amefurahia kupata mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa kimataifa ambayo yatamwezesha kuendeleza biashara yake.

 

“Kuwa mjasiriamali kunachangamoto mbalimbali, hasa kipindi ambacho biashara yako inapokuwa na changamoto. Kama mjasiriamali ni muhimu sana kujibadilisha kila wakati ili kutoa huduma bora au bidhaa bora kushindana katika soko”. Elizabeth Swai.

 

 

Hafla hiyo imehudhuriwa na wafanyabiashara takribani 40 kutoka kona mbalimbali  ndani na nje ya Tanzania akiwemo mfanyabishara wa kimataifa mwenye mafanikio makubwa bwana Robin Zimbakov ambaye aliezea safari yake ya ujasirimali, changamoto alizokutanazo hadi biashara yake kusimama.

 

 

Comments are closed.