The House of Favourite Newspapers

Chadema: Bunge Limevunja Katiba Kuomba Fedha Nje ya Bajeti

0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Vincent Mashinji akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
serikali.Mkutano ukiendelea.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Vincent Mashinji, amesema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limevunja katiba ya nchi Ibara ya 137 Kwa kuomba fedha za ziada nje ya bajeti iliyoidhinishwa na bunge bila kupitisha maombi hayo bungeni kama katiba inavyotaka.

 

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mashinji alisema:

 

‘’Kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji wa bunge ya mwaka 2008 Kifungu cha 31 kinaeleza kuwa fedha zote kwa ajili ya uendeshaji wa bunge zinawekwa kwenye mfuko maalum kama ulivyoanzishwa na sheria hiyo na msimamizi mkuu wa fedha hizo ni Katibu Mkuu wa Bunge kwa mujibu wa kupengele cha (2) na (3)cha katiba.

 

Kati ya Juni 21, 2017 na Agosti 15, 2017 Katibu wa Bunge aliandika barua tatu tofauti akiomba fedha zaidi ya shilingi bilioni tisa (9,966,464,000.00) kwa Waziri wa Fedha na kwa Katibu Mkuu wa Hazina kwa ajili ya kugharamia bajeti ya ziada na fedha za matumizi mengineyo kwa ajili ya bunge ikiwa nje ya bajeti iliyokuwa imeidhinishwa na bunge na kuwekwa katika mfuko maalum wa bunge katika mwaka wa fedha wa 2016/17.

 

Tangu wakati huo mpaka Agosti 15 mwaka huu serikali ilishatoa bajeti ya ziada kwa bunge kiasi cha shilingi bilioni 7 kutoka katika mfuko mkuu wa hazina bila kufuata masharti ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

 

Aidha aliendelea kueleza kuwa naye Waziri wa Fedha pia amevunja katiba Ibara ya 136 na 137 (3) kwa kutoa fedha za ziada nje ya bajeti iliyopitishwa na bunge kutokana na katiba inavyomtaka kuwasilisha bungeni maombi ya bajeti ya ziada au maelezo ya matumizi ya nyongeza bungeni na baada ya bunge kukubali maombi hayo ndipo ingelimbidi kuwasilisha mswada wa sheria bungeni ya matumizi ya fedha za serikali kwa ajili ya kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka mfuko mkuu wa hazina ya

Na Denis Mtima/GPL

Leave A Reply