The House of Favourite Newspapers

Chadema Hawamwamini Msimamizi Uchaguzi Kinondoni (Video)

Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila (katikati).

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo wamesema hawana imani na msimamizi wa uchaguzi jimbola Kinondoni wakidai kuna njama zilizopangwa dhidi ya chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika wiki ijayo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila,  amesema baadhi ya njama hizo ni kuwepo taarifa kwamba kuna watu walioletwa kutoka Zanzibar kuja kushiriki uchaguzi huo wa Kinondoni ambapo amesema wapo kwenye hoteli na nyumba za kulala wageni eneo la Kijitonyama, Kinondoni,  jijini Dar es Salaam.

 

Kigaila aliongeza kusemakwamba chama chake kimeona dalili za hujuma ambazo hupangwa kila unapofika wakati wa uchaguzi  ambapo watu hushambuliwa, kutekwa na kufanyiwa vitendo vibaya.

Comments are closed.