The House of Favourite Newspapers

Chadema Wafurika Mahakamani Kusubiri Dhamana ya Mbowe – Pichaz

Edward Lowassa na viongozi wengine wa Chadema wakiwa mahakamani hapo.

WAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo wamefurika katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar  wakiimba nyimbo za kutaka Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe na viongozi wenzake waachiwe.

Wafuasi wa Chadema wakiwa nje ya mahakama.

Mbowe na wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na manaibu wake wa Bara na Zanzi­bar, John Mnyika na Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wote wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo mawili ya uchochezi wa uasi yanayom­kabili Mbowe na wanatarajiwa kuachiwa kwa dhamana leo.

Wafuasi hao wamekuwa mahakamani hapo tangu mapema asubuhi  leo wakisubiri kuwalaki viongozi hao waliokaa rumande kwa siku saba tangu wiki iliyopita.

UPDATES: Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Freeman Mbowe wametimiza masharti ya dhamana katika kesi yao Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Polisi wakiimarisha ulinzi.

Aidha, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi ameomba kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ili kumjumuisha Mdee katika kesi inayowakabili viongozi wengine sita wa Chadema.

BREAKING NEWS: Mbowe na Viongozi 5 CHADEMA Waachiwa Huru

Comments are closed.