The House of Favourite Newspapers

Chadema Yamuunga Mkono Maalim Seif Zanzibar

0

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema rasmi sasa wanakiunga mkono chama cha ACT Wazalendo kwa upande wa Zanzibar katika uchaguzi Mkuu 2020, ambapo Maalim Seif Sharif Hamad anagombea Urais wa Zanzibar kupitia ACT.

 

Mgombea Urais Chadema, Tundu Lissu, amesema wamefanya uamuzi huo kutokana na historia ya Zanzibar kuwa na wanachama wengi wa CCM na ACT Wazalendo, hivyo Chadema wamechagua kuwaongezea nguvu ACT ambao ni wapinzani wenzao ili ishinde uchaguzi huo.

 

“Tunaiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ile ya Zanzibar (ZEC) kuhakikisha wanaandaa fomu za matokeo ya uchaguzi kwenye vituo ili kila wakala wa chama apate nakala,” amesema Lissu akiongeza kwamba suala hilo litapunguza mgogoro kati ya NEC, vyama vya siasa na mawakala.

Leave A Reply