The House of Favourite Newspapers

CHADEMA Yasusia Uchaguzi Ngorongoro

0

TAARIFA KWA UMMA

Katibu Mkuu John Mnyika ameiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuitaarifu rasmi kuwa Chadema hakitashiriki uchaguzi wa marudio wa ubunge kwenye Jimbo la Ngorongoro na kata saba na badala yake amesisitiza kutaka iundwe Tume Huru ya Uchaguzi itakayohakikisha chaguzi zinakuwa huru, za haki na halali kuanzia katika uchaguzi wa marudio mpaka katika uchaguzi mkuu.

 

Kupitia barua hiyo Katibu Mkuu ameitaka Tume ya Uchaguzi iwataarifu wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi katika jimbo tajwa na kata za Handali, Bomalang’ombe, Nyalubanda, Nalasi Mashariki, Likombe , Ipwani na Naumbu kutokutoa fomu wala kufanya uteuzi kwa yoyote atayetambulishwa kinyume cha katiba ya chama na barua hii kuwa ni mgombea kupitia Chadema.

 

Aidha kupitia barua hiyo Katibu Mkuu ameikumbusha kwa mara nyingine Tume ya Uchaguzi kujibu barua ya Chadema ya tarehe 25 Novemba 2020 yenye kumb. Na. C/HQ/ADM/20/TU/05/14 ambapo chama kilitaka maelezo ni nani alisaini barua na fomu za waliotangazwa kuwa wabunge viti maalum na kukipatia chama nakala ya nyaraka husika kwa ajili ya kuchukua hatua kwa kuzingatia kuwa Kamati Kuu haikuwahi kufanya uteuzi wala Katibu Mkuu hajawahi kuwasilisha orodha tajwa.

Leave A Reply