The House of Favourite Newspapers

Chalamila ataka mabasi ya Mwendokasi Kuongezewa Muda wa Kufanya Kazi

0

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amawataka Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) maarufu kwa jina la Mwendokasi, kuangalia namna ya kuongezeka muda wa kufanya kazi hadi kufikia saa 24 badala ya muda uliopo sasa.

 

Mbali na hilo pia amesema hafurahishwi na malalamiko yaliyokuwapo kwa muda mrefu juu ya kuchelewa kwa mabasi hayo jambo ambalo linawafanya wananchi kusubiri kituoni kwa zaidi ya saa 1.

 

Ametoa kauli hiyo leo Juni 27 wakati akizindua safari za mabasi hayo kati ya Gerezani hadi Mbagala rangi tatu ambayo imelenga kurahisisha huduma ya usafiri kwa watu wanaotaka kutembelea maonyesho ya sabasaba yanayotarajia kuanza kesho Julai 28, 2023.

 

Chalamila ameitaka Dart kuanza kuangalia namna ya kuongeza muda wao wa kazi ili kuhudumia watu wengi zaidi.

“Leo anzeni kuliangalia hili. Jambo ambalo sifurahishwi ni Dart kufanya kazi kwa saa kadhaa, nataka ikiwezekana wafanye kazi kwa saa 24 kama mtu ametoka saa saba akute basi kama saa 10 usiku akute basi,” amesema.

 

Amesema maana ya mwendokasi haimaanishi kufanya kazi saa 1 asubuhi hadi saa 4 usiku na kwenda kulala.

“Watu wana wagonjwa wanashindwa kupanda magari kukiwa kuna mwendokasi watapanda kwenda hospitali,” amesema.

 

Amesema mabasi yaliyosajiliwa ni mengi, huku akieleza kuwa anaamini idadi ya madereva ni mara mbili ya mabasi yaliyopo hivyo kufanya uwezekano wa kufanya kazi saa 24 kwa kupishana.

 

 

Leave A Reply