The House of Favourite Newspapers

Chalobah Asaini Mkataba Mpya Kubakia Stamford Bridge Hadi 2028

0
Mlinzi wa klabu ya Chelsea Trevoh Chalobah amesaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo hadi 2028

NYOTA wa Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza Trevoh Chalobah amesaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Stamford Bridge hadi msimu wa 2028.

 

Chalobah ambaye amekulia katika Academy ya Chelsea amepewa mkataba mpya ikiwa ni msimu wake wa pili tangu apandishwe kwenye timu ya wakubwa na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Mjerumani Thomas Tuchel.

Kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel ndiye aliyempandisha Chalobah kikosi cha kwanza kutoka kwenye Academy

Mkataba wa Chalobah una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja mbele hadi 2029, mlinzi huyo raia wa Uingereza amecheza jumla ya michezo 13 hadi sasa ndani ya msimu huu chini ya kocha Graham Potter.

 

“Nimejisikia furaha sana kusaini mkataba huu, ni heshima kubwa kila mara napovaa jezi ya klabu hii. Nataka kujitoa zaidi na kuisaidia klabu hii.” alisema Chalobah mara baada ya kusaini mkataba mpya.

Leave A Reply