The House of Favourite Newspapers

Chama Afichua Siri Ubora wa Bwalya

0

KIUNGO wa Simba na mchezaji bora wa msimu uliopita, Clatous Chama amesema kuwa siri ya ubora unaoonekana kwa kiungo mpya wa timu hiyo, Mzambia, Larry Bwalya ni kipaji kikubwa alichonacho na nidhamu yake ya kujituma mazoezini.

 

Bwalya ni miongoni mwa nyota wapya wanne wa kigeni ambao wamejiunga na Simba kwa ajili ya msimu ujao akitokea klabu ya Power Dynamos ya Zambia na kusaini mkataba wa miaka miwili.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Chama alisema: “Nimemfahamu Bwalya kabla hajajiunga na Simba, ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu na ambaye hujituma sana mazoezini.

 

“Na tangu amefi ka hapa nimekuwa nikimkumbusha kuwa amejiunga na klabu yenye malengo makubwa hivyo anapaswa kujitahidi kufi kia matarajio ambayo watu wanayo kwake.

 

”Chama msimu uliopita alihusika kwenye mabao 16 ya Simba akifunga matano na kuasisti mara 11 kwenye ligi kuu.

Leave A Reply