The House of Favourite Newspapers

Chama, Bocco wapaa Mbabane na Jeuri (Picha +Video)

KIKOSI kamili cha Simba kikiwa na mastaa kama Claytous Chama, Emmanuel Okwi, John Bocco kimeondoka alfajiri ya leo Jumapili kuelekea nchini Eswatini kikiwa na kiburi cha aina yake. Wanakwenda kurudiana na Mbabane Swallows kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema mastaa wake wakofiti na wanakwenda kumalizia kazi iliyobakia kwa kuitoa timu hiyo.

Simba itacheza na Mbabane Swallows Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Mavuso Sports Centre, Manzini nchini, Eswatini. Ikumbukwe katika mchezo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili, Aussems raia wa Ubelgiji alisema; “Tunaendakwa malengo ya kuwatoa ili tufuzu hatua inayofuata kwenye michuano hiyo hilo ndiyo jambo kubwa bila ya kuangalia matokeo yaliyopita.

“Nafahamu wapinzani wetu wakiwa kwao siyo timu rahisi, ndiyo maana nasema tutakwenda kwao kwa lengo la kuendeleza mapambano na siyo jambo lingine kwa sababu hii michuano siyo rahisi licha kuweza kupata ushindi mkubwa kwenye mchezo wa kwanza hapa nyumbani,” alisema Aussems.

Comments are closed.