The House of Favourite Newspapers

Chama, Manula Waongeza Mzuka Simba Kuelekea Michezo Mitano ya Ligi Kuu Bara

0
Kocha wa Simba Matola akiongea jambo na kiungo Clatous Chama.

 

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa, kurejea kwa mastaa wao waliokuwa kwenye majukumu ya timu za taifa akiwemo Aishi Manula, kumeongeza ari ya kikosi chao kuelekea michezo mitano iliyosalia ya Ligi Kuu Bara, huku wakitamba kukusanya pointi zote 15.

 

Mbali na waliokuwa na majukumu ya timu za taifa, pia kiungo Clatous Chama alikuwa na ruhusa maalum na tayari amerejea kambini kuungana na wenzake.

 

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba wanakamatia nafasi ya pili wakiwa na pointi 51, walizokusanya katika michezo 25 waliyocheza.

 

Michezo mitano ambayo Simba wanajiandaa nayo ni dhidi ya Mbeya City, KMC, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Mbeya Kwanza.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema: “Kikosi chetu jana (juzi) Ijumaa kilianza rasmi mazoezi ya kimbinu baada ya wachezaji wetu waliokuwa kwenye timu za taifa kurejea na kuungana na wenzao kwa ajili ya kujiandaa na michezo mitano iliyosalia.

 

“Licha ya kwamba kumekuwa na mabadiliko kadhaa kikosini, lakini wachezaji wana ari kubwa kuhakikisha wanawafuta machozi Wanasimba kwa kumaliza ligi kwa kushinda mechi zote zilizosalia.”

STORI: JOEL THOMAS

Leave A Reply